Tiketi za fainali ya Kombe la Dunia yauzwa kwa shilingi milioni 4.5

Dismas Otuke
1 Min Read

Tiketi za mechi ya fainali ya Kombe la Munia mnamo Julai 19 katika uwanja wa Metlife, mjini New York nchini Marekani ziliuzwa kwa kati ya dola 16,475 sawa na shilingi milioni 2.13 na shilingi dola 35,000, sawa na shilingi  milioni 4.5 za Kenya.

Tiketi zinazopatikana kwa sasa kwa mechi ya fainali zinauzwa kwa dola 35,000 za Marekani ama shilingi milioni 4.5 za Kenya kwa eneo la Trophy Lounge na dola 16,475 sawa na shilingi milioni 2.1 kwa tiketi za eneo la FIFA Pavilion.

Bei ya tiketi za mechi zingine zinauzwa kwa kati ya shilingi laki 2 za Kenya kwa eneo la Pavilion na shilingi 453,000 kwa zile za eneo la Pitchside.

Hata hivyo, tiketi za mechi ya kundi C kati ya Morocco na Brazil Juni 13 zimemalizika kuuzwa kwa maeneo yote ya uwanja.

Kumekuwa na malalamishi kuhusu bei ya juu ya tiketi za Kombe la Dunia, wengi wakiishutumu FIFA.

Makala ya 23 ya Kombe la Dunia yataandaliwa nchini Mexico, Marekani na Canada kati ya Juni 11 na Julai 19.

Share This Article