Mamelodi Sundowns na River Plate zaonyesha ubabe

Boniface Musotsi
1 Min Read

Klabu za Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) na River Plate (Argentina) zilidhihirisha ubabe wao katika mashindano ya klabu bingwa duniani yanayoendelea nchini Marekani baada ya kuzilambisha sakafu klabu za Ulsan na Urawa Reds mtawalia.

Kwenye nyuga hizo, Mamelodi Sundowns waliibuka na ushindi wa goli moja kwa nunge lililotiwa kimiani naye Iqraam Rayners dakika ya 36.

River Plate nao walivuna ushindi wa mabao matatu kwa moja kupitia kwa Facundo Colidio (12′), Sebastián Driussi (48′) na Maximiliano Meza (73′) huku lile la Urawa Reds likifungwa na Yūsuke Matsuo (58′).

Katika nyuga zingine, Borussia Dortmund ilitoka sare ya nunge kwa nunge dhidi ya Fluminense sawia na Monterrey dhidi ya Inter Milan waliopata sare ya goli moja kwa moja yaliyofungwa na gwiji matata Sergio Ramos (25′) na Lautaro Martínez (42′) mtawalia.

Leo Jumatano, Manchester City watakabana koo na Wydad saa moja jioni, Real Madrid dhidi ya Al Hilal saa nne usiku, Pachua na RB Salzburg watatesa nyasi saa saba usiku kisha Al Ain ifunge awamu ya kwanza ya kipute hicho dhidi ya Juventus saa kumi alfajiri.

Boniface Musotsi
+ posts
Share This Article