Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya, imetabiri kunyesha kwa mvua kubwa inayoandamana na ngurumo ya radi katika maeneo mengi katika kipindi cha siku saba zijazo.
Katika utabiri wake wa kati ya Novemba 10 na 16, mamlaka hiyo imesema mvua hiyo inatarajiwa kushuhudiwa katika maeneo mengi ya kaunti zote 47 nchini.
Aidha, utbairi huo umeashiria kuwa kaunti nyingi nchini zitapokea mvua nyakati za asubuhi.
Kaunti zitakazopokea mvua za asubuhi ni pamoja na Embu, Kajiado, Kiambu, Kirinyaga, Laikipia, Machakos, Mandera, Meru, Murang’a, Nairobi, Nyandarua, Nyeri, Tharaka-Nithi, Busia, Siaya, Kisumu, Kisii, Homa Bay, Migori, Turkana na Wajir.
Zingine ni zile za ukanda wa Pwani ikiwa ni pamoja na kaunti za Kwale, Mombasa, Kilifi, Tana River na Lamu.
Mvua za nyakati za mchana zinatarajiwa katika kaunti za Baringo, Bomet, Bungoma, Busia, Elgeyo Marakwet, Homa Bay, Kakamega, Kericho, Kisii, Kisumu, Migori, Nakuru, Nandi, Narok, Nyamira, Siaya, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Vihiga na West Pokot.
Maeneo yatakayopokea mvua nyakati za usiku ni Busia, Embu, Homa Bay, Kajiado, Kakamega, Kiambu, Kilifi, Kirinyaga, Kisumu, Kwale, Laikipia, Lamu, Machakos, Mandera, Marsabit, Meru, Migori, Mombasa, Murang’a, Nairobi, Nyandarua, Nyeri, Siaya, Tana River, Tharaka-Nithi, Vihiga na Wajir.
Aidha, mawingu yanatarajiwa kushuhudiwa katika kaunti zingine kama vile Bungoma, Baringo, Bomet, Elgeyo Marakwet, Kericho, Kisii, Garissa, Nakuru, Nandi, Narok, Nyamira, Makueni, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Kitui, Taita Taveta na West Pokot.