Serikali yatoa hatimiliki za ardhi 20,000 kwa wakazi wa Kwale

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, amesema serikali imechukua hatua hiyo, ili kutimiza ahadi ilizotoa kabla ya  Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022.

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali imetoa hatimiliki za ardhi 20,000 katika kaunti ya Kwale.

Ni afueni kwa wakazi wa kaunti ya Kwale baada ya serikali kuwapa hatimiliki za ardhi 20,773, hii ikiwa ni hatua ya kukabiliana na mzozo wa umiliki wa ardhi ambao umeghubika eneo hilo kwa muda mrefu.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, amesema serikali imechukua hatua hiyo, ili kutimiza ahadi ilizotoa kabla ya  Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022.

“Utekelezwaji wa ahadi za kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022 ili kukabiliana na mzozo wa ardhi wa kihistoria na kutokomeza swala la maskwota katika eneo la Pwani, unaendelea,” alisema Kindiki.

Wakazi walionufaika na utoaji huo wa hatimiliki za ardhi ni wa maeneo ya Mwavumbo, Dumbule, Gandini, Bofu na Busa.

Mwezi uliopita, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika eneo la Pwani, Rais William Ruto alitoa hatimiliki za ardhi 51,131 kwa wakazi wa sehemu kadhaa za Kwale.

Walioandamana na Naibu Rais kwenye hafla hiyo ni pamoja na Waziri wa Michezo, Vijana na Ubunifu Salim Mvurya, Gavana wa Kwale Fatuma Achani, wabunge Gonzi Rai (Kinango), Kassim Tandaza (Matuga), Feisal Bader (Msambweni), Kenneth Tungule (Ganze), na John Bwire (Taveta), wWawakilishi wadi na viongozi wa mashinani.

Share This Article