Naibu Rais Kithure Kindiki amesema kuwa serikali iatatoa shilingi bilioni moja kwa Shirika la kitaifa la biashara (KNTC), ili kununua mpunga kutoka wakulima wa eneo la Mwea.
Kindiki amesema mpango huo unalenga kuwalinda wakulima dhidi ya bei za rejareja zinazotolewa na wanunuzi wengi wa zao hilo.
Akizungumza Ijumaa katika eneo bunge la Mwea kaunti ya Kirinyaga,Naibu Rais amesema pesa hizo zitawezesha KTNC kununua mpunga ili kuweka akiba tosha ya chakula