Arsenal ndio mabingwa wa Ligi Kuuu ya Uingereza msimu wa mwaka 2025/2026, likiwa taji la kwanza tangu msimu wa mwaka 2003/2004.
Arsenal chini ya ukufunzi wa meneja Mikel Arteta, walitawazwa mabingwa Jumanne usiku bila kugusa mpira baada ya wapinzani wa karibu Manchester City kutoka sare ya bao moja ugenini dhidi ya Bournemouth.
City walikuwa na shinikizo kubwa kwani walifahamu fika kuwa ni ushindi pekee ambao ungewaweka kwenye kinyang’anyiro na kulazimu mabingwa kubainika Jumapili, Mei 24, wakati wa mechi za kufunga msimu.
Hata hivyo, City walijipata nyuma baada ya Eli Junior Kroupi kupachika bao la ufunguzi kwa wenyejeji.
Vijana wa Pep Guardiola walijituma na hatimaye kusawazisha kupitia kwa Erling Halaand kunako dakika ya sita ya muda wa mazidadi.
Arsenal wameshinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza mara nne sasa ikiwa ni pamoja na mwaka 1997/1998, 2001/2002 na 2003/2004.
The Gunners wanaongoza jedwali kwa pointi 82 baada ya mechi 37, wakifuatwa na Man City wenye alama 78, pointi 10 juu ya Man United iliyo ya tatu.
Arsenal wamemaliza nafasi ya pili katika misimu mitatu iliyopita nyuma ya Liverpool msimu uliopita.