Mabingwa watetezi Argentina,walenga kufunga kazi leo dhidi ya Austria

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Aergentina watarejea uwanjani Jumatatu usiku kwa mchuano wa pili wa kundi J uwanjani Texas, Marekani.

Pambano hilo litachezwa kuanzia saa mbili usiku huku timu zote zikiwa alama tatu baada ya kushinda mechi za ufunguzi.

Mshindi wa mechi hiyo atafuzu kwa raundi ya 32 bora .

Baadaye saa saba usiku Ufaransa watakuwa na miadi dhidi ya Iraq, kuanzia saa saba katika kundi I,kisha Senegal wakabiliane na Norway saa tisa alfajiri.

Jordan watafunga ratiba ya siku ya 12 dhidi ya Algeria saa kumi na mbili asubuhi.

Share This Article