Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA, limeondoa matumizi ya idadi ya mabao kama kigezo cha kutenganisha zinapotoshana kwa pointi.
Kulingana na FIFA mfumo huo mpya wa Head to Head, unatoa fursa sawa kwa timu zote za kundi moja .
Ni mara ya kwanza kwa FIFA kutumia mfumo wa Head to Head, ambao hauzingatii idadi ya mabao ambayo timu imefunga .
Mfumo huo ulitumika kwa mara ya kwanza katika fainali za Kombe la Dunia baina klabu mwaka uliopita nchini Marekani.