Kenya imezindua namba mpya ya dharura ya simu, itakayotumika kuripoti visa vya ugaidi, itikadi kali na ghasia.
Akizindua namba hiyo 0800 900 900, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, alisema wananchi sasa wataweza kutoa taarfa kuhusu vitendo vinavyoshukiwa kuwa vya kigaidi kwa urahisi na bila ya wao kujulikana, hatua itakayofanikisha vita dhidi ya ugaidi na itikadi kali hapa nchini.
Kwenya hafla hiyo, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, alielezea umuhimu wa kuimarisha imani na ushirikiano kati ya wananchi, jamii na asasi za usalama.
“Habari za mapema zinaweza zuia uharibifu, kuokoa maisha na kuhakikisha usalama katika jamii,” alisema Mudavadi.
Kulingana na Mudavadi, uzinduzi wa namba hiyo ya dharura pia umefanikisha kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na nchi ya Uingereza na Marekani, katika kuboresha mbinu za kijamii za kuzuia itikadi kali na ugaidi.
“Ushirikiano wa wananchi na asasi za usalama, unawezesha kuwa na Kenya salama, yenye amani na mahala ambapo vijana na wafanyabiashara wanastawi.