Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, amemteua tena Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na baraza hilo Mansura Mosi Kassim, uteuzi wa Othman unatekelezwa mara moja.
Othman, anatarajiwa kuapishwa Jumanne tarehe 22 September, saa nne asubuhi katika Ikulu ya Zanzibar.
Wadhifa huo ni sehemu ya Serikali ya Umoja ya Zanzibar, ambapo Makamu Rais wa Kwanza hutolewa kwenye chama cha kisiasa ambacho huibuka nafasi ya pili kwenye Uchaguzi wa Urais.
Othman Masoud ni mwanasheria mwenye taaluma ya juu na uzoefu mpana serikalini. Kabla ya kuingia rasmi katika siasa za upinzani, aliwahi kuwa Mkurugenzi mkuu wa mashtaka (2002–2011) na baadaye mwanasheria mkuu wa Serikali wa Zanzibar.