Watu wawili wafariki kwenye ajali ya ndege Kajiado

Kamanda wa Polisi wa Kajiado Moreen Kuto, alihusisha ajali hiyo na hali mbaya ya hewa, akidokeza kuwa ndege hiyo ilipoteza mwelekeo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu wawili wafariki kwenye ajali ya ndege Kajiado

Watu wawili wameaga dunia baada ya ndege walimokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la Kipeto, Kajiado Magharibi, kaunti ya Kajiado.

Akithibitisha ajali hiyo, Kamanda wa Polisi wa Kajiado Moreen Kuto, alihusisha ajali hiyo na hali mbaya ya hewa, akidokeza kuwa ndege hiyo ilipoteza mwelekeo.

Kulingana na Kuto, waliofariki ni rubani na mwanafunzi wake.

Ajali hiyo inaashiria hatari iliyopo kutokana na hali mbaya ya hewa kwa ndege ndogo, ambayo inasababisha hali ya marubani kuto-ona vizuri.

Tutakuletea habari zaidi kuhusu taarifa hiii…

Share This Article