Samia, Ndejembi wapiga kura Chamwino

Uchaguzi mdogo umefanyika Chamwino kufuatia uteuzi wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Deogratius Ndejembi, kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Marion Bosire
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepiga kura leo, Novemba 4, 2026, katika uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Chamwino, Mkoani Dodoma.

Rais Samia alipiga kura yake katika Kituo cha kupigia kura kilichopo Ofisi ya Kijiji cha Chamwino.

Uchaguzi huo unafanyika leo, kufuatia hatua ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Deogratius Ndejembi, kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi naye ameshiriki shughuli hiyo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Ndejembi alisema Wananchi wameitikia wito wa kushiriki uchaguzi huo, ambao ameuelezea kuwa huru na wa haki.

Aliongeza kuwa Mawakala wa vyama vingine vya siasa pia wamejitokeza kusimamia mchakato wa upigaji kura.

Ndejembi alipendekezwa na chama tawala CCM Agosti 27, 2026, kuchukua mahala pa Makamu wa Rais wakati huo Emmanuel Nchimbi aliyekuwa ameonyesha nia ya kung’atuka.

Bunge liliratibisha uteuzi wa Ndejembi Agosti 28, 2026 huku akiapishwa katika Ikulu ya Dodoma Agosti 29 2026.

Share This Article