Ratiba ya nusu fainali ya kombe la UEFA Nations League, imebainika baada ya kukamilika kwa marudio ya kwota fainali jana usiku.
Ufaransa, wakiwa nyumbani, waliishinda Croatia penati 5-4 baada ya mechi kuishia sare ya 2-2.
The Blues waliibwaga Croatia magoli mawili kwa bila katika mchuano wa jana na kulipiza kipigo cha 2-0 ugenini mjini Zagreb wiki jana.
Uhispania walijikatia tiketi kwa semi fainali baada ya kuwalemea Uholanzio penati 5-4, baada ya mechi kuishia sare ya 3-3 na jumla ya sare ya 5-5, baada ya mikumbo miwili.
Ureno waliishinda Denmark mabao 5-2 katika muda wa ziada baada ya mechi kumalizikia sare ya 3-3.
Denmark walishinda duru ya kwanza bao moja kwa bila huku Wareno wakishinda mechi ya marudio jana 3-2 .
Ujerumani walitoka sare ya 3-3 na Italia, lakini wakafuzu kwa nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4.
Wenyeji Ujerumani watapambana na Ureno Juni 4, katika uwanja wa Allianz Arena huku Uhispania ikiwa na miadi dhidi ya Ufaransa Juni 5 ugani Stutgart.
Fainali ya kipute hicho itasakatwa tarehe 8 mwezi Juni uwanjani Munich.