Sofapaka waishika mateka Gor Mahia

Gor wanashikilia nafasi ya tatu kwa pointi 47 kutokana na mechi 26, alama 2 nyuma ya viongozi Police FC waliosakata mchuano mmoja zaidi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Sofapaka walihitaji bao la dakika ya 90 kutoka kwa mshambulizi wa Uganda Douglas Ochoko, ili kulazimisha sare ya bao moja dhidi ya mabingwa watetezi Gor Mahia, katika mechi ya Ligi kuu FKF PL, iliyosakatwa Jumamosi uwanjani Dandora.

Joshua Onyango alikuwa amewaweka K’ogalo uongozini kunako dakika ya 68, baada ya kipindi cha kwanza kumalizikia sare kappa.

Hata hivyo mabao mawili ya Gor Mahia yalikataliwa na mwamuzi wa mechi hiyo, likiwemo lake Benson Omalla.

Gor wanashikilia nafasi ya tatu kwa pointi 47 kutokana na mechi 26, alama 2 nyuma ya viongozi Police FC, waliosakata mchuano mmoja zaidi.

Katika matokeo mengine, Mara Sugar, wakiwa nyumbani, pia wameambulia sare ya 1-1, huku Moses Shumah akipachika bao la ushindi kwa Kakamega Homeboyz, waliokuwa ugenini dhidi ya Bandari FC.

 

Website |  + posts
Share This Article