Putin asitisha vita nchini Ukraine msimu huu wa Pasaka

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Urusi Vladimir Putin, ameamrisha kusitishwa kwa shughuli zote za kijeshi nchini Ukarine hadi baada ya siku kuu ya Pasaka.

Putin hata hivyo amesema kuwa majeshi ya Urusi ni sharti yawe tayari kukabiliana na mashambulizi yoyote wakati wa sherehe hizo.

Kulingana na Putrin, vita hivyo vimesitishwa kati ya saa kumi na mbili jioni ya leo na kuendelea hadi Jumatatu saa saba adhuhuri.

Urusi inaamini kuwa Ukraine pia itafuata mkondo huo na kusitisha vita hadi baada ya sherehe hizo za Pasaka.

Haya yanajiri siku moja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kusema kuwa watajiondoa katika mazungumzo ya kuleta amani baina ya Ukraine na Urusi endapo mwafaka hautaafikiwa hivi karibuni.

Website |  + posts
Share This Article