Prof. Kithure Kindiki ateuliwa kuwa Naibu mpya wa Rais

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto amemteua Prof. Kithure Kindiki kuwa Naibu mpya wa Rais. 

Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula ametangaza hayo wakati wa kikao maalum cha bunge leo Ijumaa.

Prof. Kindiki sasa anatarajiwa kupigiwa msasa na bunge na uteuzi wake kupigiwa kura na wabunge.

Ikiwa uteuzi huo utaungwa mkono na wabunge, basi Prof. Kindiki atateuliwa rasmi na Rais Ruto kwenye wadhifa huo.

Hatua hiyo inafuatia hatua ya Bunge la Seneti kupitisha hoja maalum ya kutimuliwa kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Hadi kuteuliwa kwake kwenye wadhifa huo, Prof. Kindiki alikuwa akihudumu kama Waziri wa Usalama wa Kitaifa.

Share This Article