Rais William Ruto, amechapisha uteuzi wa mawaziri wawili na makatibu 14 kwenye gazeti rasmi la serikali.
Uteuzi huo unafuatia hatua ya bunge la kitaifa kuidhinisha kwa kauli moja uteuzi wao jana.
Mawaziri hao wawili walioteuliwa ni Geofrey Ruku wa utumishi wa umma na Hannah Cheptumo, wa masuala ya jinsia na wataanza kutekeleza majukumu yao leo baada ya kuapishwa
Makatibu 14 walioidhinishwa ni pamoja na
Jane Kere Imbunya, Regina Akoth Ombam, Cyrell Odede Wagunda, Caroline Wanjiru Karugu, Fredrick Ouma Olaga, Ahmed Abdisalan Ibrahim,Judith Nayiai Ramaita-Parenona Bonface Barasa Makokha.
Wengine ni Shaukat Ali Abdulrazak, Stephen Isaboke, Michael Lenasalon, Fikirini Jacobs Katoi Kahindi, Carren Ageng’o Achieng na Aden Abdi Millah.