Kilabu ya Arsenal ilijikatia tiketi kwa nusu fainali ya taji ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16.
Arsenal waliwatema nje mabingwa mara 15 Real Madrid baada ya kuwazabua mabao mabao 2-1 katika marudio ya kwota fainali, Bukayo Saka na Gabriel Martinelli, wakifunga mabao ya wageni huku Vinicius Junior, akipachika bao pekee kwa wenyeji.
The Gunners walifuzu kwa nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1 kufuatia ushindi wa 3-0 katika mkondo wa kwanza.
Inter Milan ilifuzi pia kwa nusu fainali licha ya sare ya 2-2 na Bayern Munich, wakisajili suhindo wa jumla wa 4-3.
Arsenal itachuana na PSG katika nusu fainali Aprili 29 huku Inter Milan,wakiwa na miadi na Barcelona.