Diamond Platnumz awasili Nigeria kwa harusi ya Jux

Harusi hiyo ya kitamaduni inafanyika leo.

Marion Bosire
1 Min Read

Msanii wa muziki nchini Tanzania Diamond Platnumz yuko nchini Nigeria kwa ajili ya harusi ya kitamaduni ya mwanamuziki mwenza Juma Jux na mkewe Priscilla Ojo ambayo inafanyika leo Aprili 17, 2025.

Mapema leo, mwanamuziki huyo alichapisha video ambazo zinamwonyesha akielekea uwanja wa ndege na kuabiri ndege kuelekea Lagos Nigeria kwa ajili ya hafla hiyo.

Diamond alikuwa ameandamana na watu kadhaa akiwemo mwanamuziki Ommy Dimpoz.

Bwana harusi Juma Jux aliwasili Lagos jana kwa hafla ya leo lakini alikuwa huko siku chache zilizopita kwa ajili ya kongamano la muziki.

Wanamitandao wanasubiri kwa hamu kujionea machapisho ya matukio katika hafla ya wapenzi hao wawili ambao wanakamilisha awamu ya Nigeria ya kufunga ndoa baada ya kumaliza awamu ya Tanzania.

Priscilla Ojo ni mzaliwa wa Nigeria na ni binti ya mwigizaji maarufu wa Nollywood Iyabo Ojo.

Website |  + posts
Share This Article