Bunge latupilia mbali hoja ya kwanza ya kumtimua Spika Wetang’ula

Dismas Otuke
1 Min Read
Moses Wetang'ula - Spika wa Bunge la Taifa

Bunge la kitaifa limetupilia mbali pendekezo la kwanza la kumtimua Spika wa bunge hilo Moses Wetang’ula kwa madai ya kukiuka sheria.

Yamkini Karani wa bunge la kitaifa Samuel Njoroge, alipokea hoja hiyo Februari 7 mwaka huu.

Hata hivyo, hoja hiyo imetupiliwa mbali kwa kutofuata taratibu ufaao.

Hii inafuatia hatua ya zaidi ya wabunge 35 wa muungano wa Azimio waliojawa na hamaki kutishia kumng’atua spika Wetang’ula, baada ya Mahakama Kuu kuamuru kuwa Azimio, ndio muungano wenye idadi kubwa ya wabunge kinyume na uwamuzi wa Spika huyo aliyesema kuwa Kenya Kwanza ndio muungano wenye wabunge wengi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *