Starlets yaimarisha mazoezi kuikabili Tunisia

Dismas Otuke
1 Min Read

Vivian Nasaka, anayesakata soka ya kulipwa nchini Uturuki, atakuwa mchezaji wa mwisho wa kulipwa kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Harambee Starlets, kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake mwaka 2026 dhidi ya Tunisia.

Nasaka, anayepiga soka ya kulipwa na kilabu cha Hakkarigucu nchini Uturuki, atawasili humu nchini tarehe 19 mwezi huu akiwa mchezaji wa mwisho kati ya wachezaji 16 wa kulipwa waliojumwishwa kwenye timu hiyo ya Starlets.

Starlets chini ya kocha Beldine Odemba, itakayocheza mkondo wa pili Jumanne juma lijalo, itakuwa ikitafuta ushindi kwenye mkondo wa kwanza kabla ya kuelekea nchini Tunisia, huku ikitafuta nafasi kwenye makala ya mwaka 2026 ya bara Afrika, baada ya kukosa nafasi kwenye fainali za mwaka 2024.

Fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake mwaka 2026 zitaandaliwa mwezi Machi nchini Morocco, miezi minane baada ya makala yaliyoaihirishwa ya mwaka 2024 yatakayochezwa mwezi Julai mwaka huu nchini Morocco.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *