Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi ametUMA risala za rambirambi kufuatia kifo cha mbunge wa Malava Moses Malulu Injendi.
Mudavadi ametaja kifo hicho kuwa pigo kubwa kwa taifa na pia kwa wakazi wa eneo bunge la Malava.
Mudavadi ametaja kuwa kifo cha Mbunge huyo kama kile ambacho kimeacha pengo kubwa.
Kifo cha Mbunge huyo aliyekuwa akihudumu kwa muhula wa tatu kimetangazwa na Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula siku ya Jumatatu jioni.
Mbunge huyo alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi.