Ndoto ya timu za Kenya Pipeline na Kenya Commercial Bank kucheza fainali ya Voliboli ya kilabu bingwa Afrika ilizimwa Ijumaa usiku, baada ya kupoteza kwa wenyeji Misri katika makala ya 37.
Kenya Pipeline walishindwa na wenyeji Al Ahly ya Misri kwa seti 3-1 za 25-15,19-25,25-18,na 5-13 wakati KCB wakizidiwa maarifa na Zamalek pia ya Misri kwa seti zizo hizo 3-1 za 25-22,12-25,11-25 na 21-25 .
KCB na Pipeline watapambana katika mechi ya kuwania nishani ya shaba Jumamosi jioni kabla ya kupisha fainali kati ya Ahly na Zamalek.