Ndemo akataa uteuzi wa chuo Kikuu cha Nairobi

Kupitia ukurasa wa Facebook,Ndemo amesema amekataa uteuzi huo na alijiondoa kuwania wadhfa huo baada ya kubaini kuwa utaratibu ufaao haukufuatwa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Balozi wa Kenya nchini Ubelgiji, Profesa Bitange Ndemo, amekataa uteuzi wa kuwa Naibu Chansela wa chuo Kikuu cha Nairobi, uliotangazwa na halmashauri ya chuo hicho.

Baraza la chuo kikuu cha Nairobi kupitia kwa mwenyekiti wake lilimtangaza Profesa Ndemo kuwa Naibu Chansela kutwaa nafasi ya kaimu naibu Chansela Profesa Margaret Jesang.

Kupitia ukurasa wa Facebook,Ndemo amesema amekataa uteuzi huo na alijiondoa kuwania wadhfa huo baada ya kubaini kuwa utaratibu ufaao haukufuatwa.

Ndemo amesisitiza kuwa jina lake lilikuwa miongoni mwa majina matatu ya mwisho ya wanaotaka kazi hiyo licha yake kujindoa mapema.

Hatua ya Ndemo ambaye anayeelekea kukamilisha muda wake wa kuhudumu katika ubalozi wa Kenya nchini Ubelgiji inatarajiwa kuzua mzozo wa uongozi katika chuo kikuu cha Nairobi.

Website |  + posts
Share This Article