Moto uliozuka katika mbuga za wanyamapori wazimwa

Dismas Otuke
1 Min Read
Baadhi ya mbuga za kitaifa hapa nchini zinateketea.

Moto uliozuka katika baadhi ya mbuga za wanyamapori nchini umezimwa.

Moto uliozuka Ijumaa usiku katika buga ya kitaifa ya wanyamapori ya Nairobi uliathiri zaidi ya ekari 210, kati ya ekari 28,000 za mbuga hiyo.

Akizuru mbuga hiyo siku ya Ijumaa waziri wa utalii Rebecca Miano, alisema moto huo huenda ulisababishwa na watu waliokuwa wakivuta sigara, kurina asali au kuchoma msitu.

Maafisa wa huduma ya misitu nchini wamekuwa wakipambana na moto katika hifadhi za wanyamapori za Aberdare Forest, Ruma National Park katika kaunti ya Homa Bay, na South Island National Park eneo la Loiyangalani, kaunti ya Marsabit.

Mbuga za kitaifa za wanyama za mlima Elgon na Tsavo West pia ziliripoti mioto.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article