Wizara ya Fedha imekanusha madai kuwa shilingi trilioni 1.3 zilitolewa kwenye akaunti katika kipindi miezi saba iliyopita.
Katibu katika Wizara hiyo Dkt. Chris Kiptoo amesema kuwa hela zote zinatolewa kwenye akaunti ni sharti zifuate utaratibu uliowekwa.
Dkt. Kiptoo amekariri kuwa wizara hiyo hufanya shughuli zote za kuhamisha pesa au kutoa malipo kwa uwazi na uwajibikaji.
Taafira hiyo ilikuwa ya kuzima uvumi uliozagaa mitandaoni na katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa shilingi trilioni 1.3, za wizara zilitolewa kwenye akaunti katika muda wa miezi saba iliyopita.