Maombi ya 23 ya kitaifa yataandaliwa Alhamisi Mei 27, 2026, katika hoteli ya Safari Park Jijini Nairobi.
Hafla hiyo itaongozwa na Rais William Ruto, wabunge wa Senate na wale wa Bunge la Taifa pamoja na wageni wengine waalikwa.
Maombi hayo ya kitaifa huandaliwa kila Alhamisi ya mwisho wa mwezi wa Mei.
Lengo la maombi hayo ni kuliombea taifa, kuimarisha utangamano na kufanikisha ushirikiano wa viongozi mbali mbali kutoka kwa jamii.
Maombi hayo huandaliwa chini ya uongozi wa Maspika wa Senate na Bunge la Taifa pamoja na kamati andalizi ya hafla hiyo.
Aidha, yataandaliwa siku moja baada ya kongamano la wanawake litakaloandaliwa Jumatano Mei 27 2026.