Watu watatu wafariki baada ya ndovu kusababisha ajali Uganda

Gari hilo lilikuwa limewabeba maafisa saba kutoka mamlaka ya kukusanya ushuru nchini Uganda (URA).

Tom Mathinji
1 Min Read

Watu watatu wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari walimokuwa wakisafiria kumgonga ndovu na kusababisha ajali ya barabarani katika mbuga ya wanyamapori ya Murchison Falls nchini Uganda.

Kulingana na Jeshi la Polisi la Uganda, gari hilo aina ya Toyota Hiace, lilikuwa limewabeba maafisa wa Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru ya Uganda (URA) ajali hiyo ilipotokea.

“Abiria watatu walifariki papo hapo, huku wengine wanne akiwemo dereva wa gari hilo wakipata majeraha,” lilisema Jeshi hilo la Polisi kwenye taarifa.

Polisi walisema miili ya waliofariki ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Anaka, ikisubiri upasuaji.

“Madereva wanahimizwa kuwa waangalifu zaidi wanapopita katika mbuga hususan nyakati za usiku na kuzingatia mwendokasi uliowekwa ili kuzuia ajali kama hizo,” iliongeza taarifa hiyo ya polisi.

Share This Article