Mshukiwa wa mauaji ya watoto wanne wa chekechea nchini Uganda Christopher Okello Onyum, amefikishwa mahakamani na kukanusha mashtaka dhidi yake.
Onyuma anadaiwa kuwaua kwa kuwadunga kisu watoto wanne katika shule moja ya chekechea Jijini Kampala Aprili 2, 2026, na alikamatwa alipokuwa akijaribu kutoroka eneo la mkasa.
Licha ya viongozi wa mashtaka kusema kuwa mshukiwa huyo alikiri kutekeleza mauaji hayo, alipofikishwa mahakamani Onyuma alikanusha mashtaka yote manne dhidi yake.
“Ninakanusha mashtaka hayo,” Onyum aliambia mahakama moja ya Kampala.
Watoto waliouawa walikuwa wa umri wa kati ya miaka miwili na minne.
Watoto hao waliouawa ni pamoja na Eteku Gideon, Kaise Alungat, Ignatius Sserwange na Ryan Odeke