Maafisa 2 wa polisi wauawa katika shambulizi Garissa

Hii ni baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi cha kujitengenezea, IED kinachoshukiwa kuwekwa barabarani na wanamgambo wa Al - Shabaab.

KBC Digital News
1 Min Read

Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Fafi Stephen Ekirapa na dereva wake walifariki leo Ijumaa asubuhi baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi cha kujitengenezea (IED). 

Kilipuzi hicho kinashukiwa kuwekwa barabarani na wanamgambo wa Al – Shabaab.

Kwa mujibu wa kamanda wa kaunti ya Garissa Samson Chelugho aliyethibitisha kisa hicho, wawili hao walikuwa akisafiri kuelekea  Garissa kwenye barabara ya Dadaab wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi hicho.

Wawili hao walifariki papo hapo na gari kuharibika kabisa.

Polisi mjini Garissa wameanzisha uchunguzi katika eneo la ajali wakati wakiwasaka wanamgambo hao.

Taarifa ya KNA

Share This Article