Idadi ya watoto wanaofariki kutokana na Ebola yaongezeka DRC

Kulingana na afisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia maswala ya Kibinadamu (OCHA), watoto na kina mama ndio wanaoendelea kuathiriwa zaidi na chamko la Ebola katika mkoa wa Ituri.

Tom Mathinji
1 Min Read
Idadi ya watoto wanaofariki na Ebola yaendelea kuongezeka DRC.

Watoto zaidi ya 300 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa wa Ebola, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Habari hizo zimethibitishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa, huku wataalam wa afya wakitoa wito wa kuanza kutumiwa kwa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa huo ili kuzuia maambukizi zaidi ya aina hiyo ya Ebola ya Bundibugyo.

Kulingana na afisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia maswala ya Kibinadamu (OCHA), watoto na kina mama ndio wanaoendelea kuathiriwa zaidi na chamko la Ebola katika mkoa wa Ituri.

Janga la Ebola linaendelea kuwakosesha watu usingizi katika mkoa wa Ituri, ambapo takriban watu milioni moja wameachwa bila makwao, kutokana na ghasia zinazoshuhudiwa.

Kwa mujibu wa OCHA, watoto wanajumuisha robo moja ya vifo vyote vinavyohusishwa na Ebola nchini DRC, ikidokeza kuwa chamko hilo limesambaratisha pia utoaji huduma muhimu za afya.

Watafiti wamesema kuwa chanjo ya kukabiliana na aina hiyo ya Bundibugyo, ndio suluhisho la pekee wakati huu.

TAGGED:
Share This Article