KWS imeimarisha juhuzi za kumtafuta Fisi aliyeonekana Syokimau

Tom Mathinji
1 Min Read
KWS wanamtafuta Fisi aliyeonekana Syokimau.

Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini Kenya (KWS), limeimarisha juhudi za kumtafuta Fisi aliyeonekana siku ya Jumapili katika eneo la Syokimau kaunti ya Machakos.

Kupitia kwa taarifa, KWS imesema imewatuma maafisa wake kwenye eneo hilo, huku ishara za awali zikidokeza mnyama huyo wa mwituni anatembea katika maeneo yaliyo na vichaka, na sehemu iliyotengwa karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, akielekea eneo la Katani.

“ Tunawahakikishia wakazi wa Syokimau na maeneo yaliyo karibu kuwa operesheni ya kumtafuta fisi aliyeonekana Jumapili Mei 10, 2026, inaendelea,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

KWS imetoa wito kwa wakazi kuwa watulivu na pia kuepuka aliko mnyama huyo, kuwalinda watoto wao na kutoa ripoti mara moja kwa shirika hilo, ikiwa watamwona.

“KWS imejitolea kulinda maisha ya binadamu  pamoja na wanayamapori,” iliongeza taarifa hiyo.

TAGGED:
Share This Article