Rais Ruto: Kenya inachukua hatua muhimu kufanikisha utengenezaji wa dawa

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Kenya William Ruto.

Rais wa Kenya William Ruto, amesema taifa hilo la Afrika Mashariki, linachukua hatua madhubuti kufanikisha upatikanaji wa bidhaa za dawa.

Kiongozi huyo wa nchi alisema hatua hizo zinajumuisha kuwezesha Halmashauri ya Taifa ya Udhitibi, kuafikia kiwango cha 3 cha Shirika la Afya Duniani (WHO), ili kuhakikisha ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa zinazotengenezewa nchini Kenya.

“Lengo letu ni kuiweka Kenya kuwa kitovu cha kanda hii kwa utenegenezaji wa dawa, uvumbuzi katika sekta ya Afya na usambazaji wa bidhaa za dawa nchini Kenya na katika masoko ya Afrika,” alisema Rais Ruto.

Rais Ruto alisema Afrika hawezi endelea tena kutegemea dawa kutoka nje ya bara hilo, akidokeza kuwa Afrika hukabiliwa na asilimia 25 ya magionjwa, lakini hutengeneza chini ya asilimia sita ya dawa.

Alielezea umuhimu wa Afrika kuwa na mifumo thabiti na ya kujitegemea katika kukabiliana na dharura za kimatibabu, pamoja na kubuni nafasi za ajira, ukuaji wa viwanda na kuimarisha ukuaji wa uchumi.

Aliyasema hayo siku ya Jumanne, wakati wa mkutano kuhusu utengenezaji na upatikanaji wa dawa (AIM2030), kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Africa Forward, Jijini Nairobi.

TAGGED:
Share This Article