Koskei azitaka asasi za serikali kufanya kazi kama kitu kimoja

Martin Mwanje
2 Min Read
Felix Koskei - Mkuu wa Utumishi wa Umma

Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei ametoa wito kwa Wizara, Idara na Mashirika ya Serikali kufanya kazi pamoja kama serikali moja ili kuboresha utoaji huduma kwa raia.

Kwa upande mwingine, Koskei amewataka maafisa wa uhasibu kuhakikisha mawasiliano mujaribu ya hatua zinazopigwa katika utekelezaji a miradi ya serikali kupitia ushahidi unaoweza kuthibitishwa.

Kwa kufanya hivi, Koskei anasema hatua hiyo itachangia mazungumzo ya kitaifa juu ya mustakabali wa nchi baada ya Ruwaza ya Mwaka 2030.

Mkuu huyo wa Utumishi wa Umma aliyasema hayo leo Jumatano alipoongoza mkutano wa mashauriano kwa njia ya mtandao uliowaleta pamoja Makatibu, Wenyeviti na Maafisa Wakuu Watendaji wa mashirika ya serikali.

Maafisa hao wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza sera za serikali ili kuzifanywa kuwa mipango, miradi na huduma ambazo zina athari ya moja kwa moja kwa Wakenya.

“Mashauriano yetu yalihusu kaulimbiu ‘Kumaliza kwa Kishindo kupitia Usimamizi Madhubuti na wenye Dhamira’, yakiangazia uboreshaji wa uratibu, uongezaji kasi ya uratibu na kuhakikisha kwamba mipangob ya serikali inaafikia matokeo yaliyokusudiwa,” alisema Koskei kwenye taarifa.

“Maafisa wa uhasibu watatekeleza mapitio mapana ya miradi, mipango na maagizo katika idara zao husika na kuweka pamoja hadhi zao ndani ya wiki mbili.”

Koskei anasema hatua hiyo itasaidia kutoa taswira kamili ya utekelezaji wa miradi ya serikali, kuainisha rasilimali na kuangazia nyanja ambazo mamlaka na majukumu yanaingiliana.

 

 

 

Share This Article