Wakenya wameshauriwa kutahadhari dhidi ya mvua kubwa inayotarajiwa nchini kwa juma moja lijalo .
Idara ya utabiri wa hali ya anga imetangaza kuwa viwango vya mvua kubwa vinavyotarajiwa baina ya Jumamosi Aprili 13 na Alhamisi tarehe 18.
Maeneo yanayotarajia mvua kubwa ni ukanda wa Ziwa Victoria,bonde la ufa,Nairobi na pwani.
Mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hewa
David Gikungu amesema kuna uwezekano wa mvua hiyo kuandamana na ukungu na mafuriko.
Kaunti zinazotarajia mvua kubwa ni:-Kisumu, Homabay, Siaya, Migori, Busia, Kisii, Nyamira, Nandi, Kericho, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Narok, Baringo, Nakuru, Trans-Nzoia, Uasin- Gishu, Elgeyo-Marakwet, West-Pokot na Nyandarua.
Kaunti nyingine ni OLaikipia, Nyeri, Kirinyaga, Murang’a, Kiambu, Meru, Embu, Tharaka-Nithi, Nairobi, Machakos, Kitui, Makueni, Kajiado, Taita- Taveta, Mombasa, Tana-River, Kilifi, Lamu, Kwale, Marsabit, Garissa na Isiolo.
Gikungu amewashauri madereva kuwa makini na kutoendesha magari ndani ya mafuriko.