Gloria Bugie atizamia kuandaa tamasha ya kwanza 02 Arena

Anadai mashabiki wa nyumbani tayari wamemkera ndiposa anapeleka tamasha yake Uingereza.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki chipukizi wa Uganda Gloria Bugie ameshangaza wengi baada ya kusema angependa kuandaa tamasha yake ya kwana kabisa nje ya nchi hiyo.

Bugie ambaye amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa takribani miaka miwili pekee, amekuwa akishinikizwa na mashabiki aandae tamasha ya kibinafsi ya kwanza kabisa.

Kufikia sasa, mwanamuziki huyo ametoa nyimbo zinazoweza kukidhi tumbuizo la zaidi ya lisaa limoja jukwaani na hata ingawa amekuwa akikabiliwa na ukosoaji, amesalia kuwa msanii aliyejitolea kusukuma taaluma yake kwa viwango vikubwa.

Akizungumza alipokuwa akitagusana na mashabiki kwenye TikTok mubashara, Gloria Bugie alikasirishwa na shabiki aliyeuliza kuhusu siku ambayo ataandaa tamasha yake.

Bugie alimjibu akisema kwamba mashabiki wa nyumbani tayari wamemkera kuhusiana na jinsi walichukulia mwonekano wake na hulka yake kwenye kikao na wanahabari akiwa na nyota wa muziki wa Tanzania Diamond Platnumz.

Kutokana na hilo, mrembo huyo alisema ameamua kutoandaa tamasha yake nchini Uganda na badala yake ataipeleka kwenye uwanja wa 02 Arena jijini London, nchini Uingereza.

Diamond alikuwa amewasili jijini Kampala Alhamisi Oktoba 29, 2036, jioni kwa ajili ya kutumbuiza kwenye hafla ya kusherehekea miaka 10 ya tamasha ya vichekesho ya Comedy Store.

Katika mkutano wa wanahabari wa kumkaribisha Diamond, Bugie alionekana akimwomba ampige pambaja na kuzua gumzo.

Share This Article