Kasanga achaguliwa mwenyekiti wa bodi ya KAMP

Alichaguliwa Kwenye mkutano mkuu wa mwaka huu wa 2026 wa shirika hilo ambao pia ulijumuisha uchaguzi wa wanachama wa bodi.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili nchini Kenya Japheth Kasanga,amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la usimamizi wa pamoja wa hakimiliki la Kenya Association of Music Producers,KAMP.

Haya yalifanyika katika mkutano mkuu wa mwaka huu wa 2026 wa shirika hilo ambao pia ulijumuisha uchaguzi wa wanachama wa bodi ya shirika hilo.

Kasanga ana tajriba ya zaidi ya miaka 35 katika utayarishaji wa muziki, uchapishaji wa kazi za muziki na usimamizi wa hakimiliki, ambayo anakuja nayo katika nafasi hiyo ya uongozi.

Uchaguzi wake unatarajiwa kufungua ukurasa mpya unaolenga kuimarisha utawala wa shirika, kutetea haki za watayarishaji wa muziki na kuboresha shughuli za KAMP za usimamizi wa pamoja wa hakimiliki.

Katika kumpongeza mwenyekiti huyo mpya, KAMP ilieleza imani yake katika uongozi wake na kumtakia yeye pamoja na wajumbe wapya wa bodi mafanikio wanapoanza kutekeleza majukumu yao mapya.

Share This Article