Tume Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), inaimarisha ushirikiano wake na Shirika la Umoja wa Mataifa Kukabiliana na Ufisadi na uhalifu wa kiuchumi.
Haya yalitangazwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC Abdi Mohamud kufuatia mkutano na Mkurugenzi Mkuu wa Afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mihadarati na Uhalifu (UNODC), Dkt. Monica Juma, jijini Vienna, Austria.
Mazungumzo hayo yaliangazia kuimarisha utekelezaji sheria, utumizi wa teknolojia na usaidizi wa kisheria wa pamoja kati ya Mataifa ya Afrika Mashariki.
“ Maswala hayo ni muhimu katika kushughulikia kushughulikia Ufisadi na kulinda rasilimali za umma,” alisema Mohamud.
Mohamud alipongeza afisi ya UNODC kwa kuipiga jeki EACC kupitia usaidizi wa kisheria na misaada ya kibinadamu nchini Kenya (PLEAD) na kitovu cha UNODC barani Afrika kilicho Nairobi
Mohamud pia alimuatifu Dkt. Juma kuhusu kubuniwa kwa Kituo cha Utafiti na Mafunzo dhidi ya Ufisadi (CEREAC) Jijini Nairobi, huku akitoa wito kwa UNODC kusaidia katika juhudi hizo.