Makala ya 10 ya fainali za Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17, yataanza kutifua vumbi leo Jumamosi Oktoba 17 nchini Morocco.
Mataifa 24 yaliyotenganishwa katika makundi sita ya timu nnne nne , kutoka mabara yote yatawania taji hiyo huku fainali yake ikisakatwa tarehe 7 mwezi ujao.
Kundi A linajumuisha wenyeji Morocco,New Zealand,Ujerumani na Argentina wakati kundi B likisheheni Poland,Nigeria,mabingwa watetezi Korea Kaskazini na Puerto Rico.
Mechi nne zitapigwa leo Ujermani wakikumbana na Argentina katika mechi ya ufunguzi kundini A ,huku mabingwa watetezi Korea Kaskazini, wakianza kibarua na PPublic rto Rico katika kundi B.

Wenyeji Morocco watakabiliana na New Zealand katika mchuano wa tatu ambao pia utakuwa na sherehe za ufunguzi nao Nigeria wafunge siku katika mechi ya kundi B dhidi ya Poland.
Brazil,Norway,Canada na Ghana zimo kundi C huku Ufaransa,Venezuela,Japan na Zambia wakiwa kundi D.
Kenya wanaoshiriki kwa mara ya pili wamo kundi E pamoja na Marekani,Uchina na Samoa huku Uhispania,Chile,Mexico na Australia zikiunda kundi la mwisho la F.