Ligi Kuu ya Kenya msimu wa mwaka 2026/2027 itaingia mechi za mzunguko wa pili siku ya Jumamosi kwa jumla ya mechi mbili zilizoratibiwa.
Kenya commercial Bank watawaalika Mathare United katika uwanja wa Police Sacco kuanzia saa tisa alasiri huku mabingwa watetezi Gor Mahia, wakizuru Homa Bay ,kuchuana na APS Bomet katika uwanja wa Raila Odinga.
Mechi tatu zaidi zitaandaliwa Jumapili,Kakamega Homeboyz wakiwa nyumbani dhidi ya Ulinzi Stars kiwarani Bukhungu,Nairobi United waizuru Shabana FC, katika uga wa Afraha kaunti ya Nakuru, kisha Murang’a Seal, iwaalike matarishi Posta Rangers.
Michuano miwili zaidi itasakatwa Jumatatu na mmoja Jumanne.