Makala ya kwanza ya mashindano ya ndondi bara Afrika yameanza Jumamosi Oktoba 17, katika ukumbi wa Kasarani huku yakiwashirikisha mabondia kutoka mataifa 15 .
Kenya inajumuisha kikosi cha Wanamasumbwi 29,wanaume 17 na wanawake 12 watakaoshindana katika uzani mbali mbali.
Hit Squad inavyojulikana timu ya Kenya ikiongozwa na nahodha Boniface Mugunde inatumaini kufanya vyema mbele ya mashabiki wa nyumbani.
Jumla ya mapigano saba yameratibiwa Jumamosi ambapo katika uzani wa unyoya kati ya kilo 50-55 wanaume,Lateef Qudus wa Nigeria tazichapa na Ntabanganiymana wa Rwanda huku Noel Luemba wa Angola akipagana na Emmanuel Ovhambu wa Kenya kisha Samuel Msubuga wa Uganda apambane na Osias Agboteney wa Benin.
katika uzani wa kadri baina ya kilo 60-65 Mateo Houinon wa Benin atashuka ulingoni dhidi ya Ismael Bekhsis wa Angola,Innocent Amoko wa Uganda amenyane na Vincent Aloice wa Kenya kisha Omar Jagana wa Gambia amalize udhia na Abuldulwahab Abulbulramon wa Niger.