Papa Leo kuondoka hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji

Leo anatarajiwa kuongoza maombi katika ukumbi wa St. Peter’s Square siku ya Jumapili, hii ikiwa hafla yake ya kwanza ya umma tangu alipolazwa hospitalini.

Tom Mathinji
1 Min Read
Pope Leo XIV.

Pope Leo XIV, anatarajiwa kuondoka hospitalini Jumamosi alasiri baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye moja ya mapafu yake, hayo yametangwa na Vatican.

Kupitia kwa taarifa, Vatican ilisema Leo alifanyiwa uchunguzi wa damu na kifua Jumamosi asubuhi, na kuashiria kwamba hali yake ya kiafya inamruhusu kwenda kuondoka hospitalini.

Leo anatarajiwa kuongoza maombi katika ukumbi wa St. Peter’s Square siku ya Jumapili, hii ikiwa hafla yake ya kwanza ya umma tangu alipolazwa hospitalini.

Kitengo cha habari cha afisi yake, kilitoa picha siku ya Ijumaa kumuonyesha Leo alisherehekea misa ya kibinafsi katika hospitali ya Gemelli.  Misa hiyo ilihudhuriwa na wahudumu wa afya pamoja na maafisa wa Vatican.

Leo mwenye umri wa miaka 71 aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu, huku madaktari wakiondoa uvimbe kwenye pafu lake la kulia katika hospitali ya Gemelli Jijini Italia siku ya Jumanne.

Madaktari wa Leo walisema upasuaji huo ulifua dafu bila changamoto zozote.

Share This Article