FIFA World Cup: Kazi ipo Simba wa Teranga wakikabana koo na Ufaransa leo

Ni mara ya pili katika historia kwa Senegal kufungua mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Teranga Lions ya Senegal itakuwa na kibarua cha ziada Jumanne usiku itakapofungua mechi za kundi I za Kombe la Dunia dhidi ya mabingwa mara mbili Ufaransa.

Pambano hilo litakalosakatwa uagni Metlife litaanza saa nne usiku huku Senegal, ambayo ni ya pili bora Afrika ikilenga kuanza vyema .

Ni mara ya pili katika historia kwa Senegal kufungua mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa ,baada ya kuwapiga le Blues, bao moja kwa bila mwaka 2002,ukiwa ushindi wa pekee dhidi ya wakoloni wao.

Baadaye saa saba usiku Norway watakuwa uwanjani Gillete kupimana nguvu na Iraq katika mchuano mwingine wa kundi hilo.

Mabingwa watetezi Argentina watachuana na Algeria kundini J katika uwanja wa Kansas kuanzia saa kumi alfajiri kesho kabla ya Austria kumaliza udhia na Jordan katika uchanjaa wa St. Clara.

Share This Article