Waziri wa Elimu Julius Ogamba, ameagiza tume ya kuwaajiri walimu (TSC), kumwadhibu Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya Alliance kwa kuongeza karo.
Aidha, Ogamba ameamrisha kuvunjwa kwa halmashauri ya shule hiyo na kutaka kufunguliwa mashtaka kwa Mwalimu mkuu Margaret Njeru, kwa kuongeza karo kinyume cha sheria na matumizi mabaya ya fedha .
Ogamba jana aliamrisha kufanywa kwa uchunguzi wa kashfa hiyo na ripoti kuwasilishwa katika afisi yake.
Hatua hiyo inafuatia malalamishi kutoka kwa baadhi ya wazazi, kuhusu kuongezwa kiholela kwa karo kwa shule nyingi za umma.