Kenya hupoteza shilingi bilioni 71 kwa uuzaji pombe ghushi

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya hupoteza takriban shilingi bilioni 71 kila mwaka kutokana na uuzaji na usambazaji wa pombe ghushi.

Kulingana na Mamlaka ya  kukabiliana na bidhaa ghushi nchini- ACA, pombe haramu na ghushi huchangia asilimia 59, ya pombe yote  inayouzwa nchini Kenya.

Afisa mkuu mtendajiwa ACA, Robi King’a, akifika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa Jumatano wiki hii alitaja mianya inayotumika kusafirisha pombe hiyo ghushi inapatikana Isibania na Shimoni katika mpaka wa Kenya na Tanzania, Mbale na Busia katika mpaka wa Kenya na Uganda na Moyale katika mpaka wa Kenya na Ethiopia.

Kulingana na King’a, pombe ghushi husafirishwa kwa kupakiwa ndani ya bidhaa nyingine ,na kutumia pikipiki kuvuka mipaka ya Kenya.

Share This Article