Serikali kujenga soko la pili la kisasa Pokot Magharibi

Hatua hiyo ilijiri ili kukimu idadi kubwa ya wafanyabiashara inayoongezeka katika eneo hilo, ikizingatiwa soko la Makutano litawafungia nje baadhi ya wafanyabiashara.

Tom Mathinji
1 Min Read
Pokot Magharibi kupoata sokomla pili la kisasa.

Serikali itawekeza shilingi milioni 300 katika ujenzi wa soko la pili la kisasa katika kaunti ya Pokot Magharibi Januari 2027, baada ya wasiwasi kuibuliwa kuwa soko la Makutano linalojengwa halitaweza kukimu idadi kubwa ya wafanyabiashara.

Rais  William Ruto alitangaza nyongeza ya uwekezaji huo baada ya kukadiria ujenzi wa soko la kisasa la Makutano katika eneo bunge la Kapenguria unalogharimu shilingi milioni 147, kwenye zira yake ya maendeleo katika kaunti ya Pokot Magharibi.

Ujenzi wa soko la Makutano umekamilika asilimia 69, ukitarajiwa kukamilika kikamilifu mwezi Disemba mwaka huu.

Hatua hiyo ilijiri ili kukimu idadi kubwa ya wafanyabiashara inayoongezeka katika eneo hilo, ikizingatiwa soko la Makutano litawafungia nje baadhi ya wafanyabiashara.

Soko hilo ni sehemu ya uwekezaji mpana wa serikali katika kaunti ya Pokot Magharibi, unaojumuisha ujenzi wa barabara, nyumba za gharana nafuu na uunganishaji wa umeme.

Share This Article