Duale akutana na maafisa wa KMPDU, aahidi kulinda haki za wahudumu wa afya

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri wa Afya Aden Duale wakati alipokutana na maafisa wa KMPDU

Waziri wa Afya Aden Duale ameahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha haki za wahudumu wa afya humu nchini zinalindwa. 

Duale amesema hatua hiyo itasaidia kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa raia kote nchini na hivyo kufanikisha mpango wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wote.

Waziri aliyasema hayo alipokutana na maafisa wa Chama cha Madaktari nchini, KMPDU ofisini mwake leo Alhamisi.

Wakati wa mkutano huo, wote hao waliangazia hatua iliyopigwa katika kutekeleza makubaliano ya kurejea kazini yaliyofikiwa kati ya wizara na chama hicho mwaka jana.

Waziri huyo aliwahakikishia maafisa hao kuwa Wizara yake itatekeleza kikamilifu makubaliano hayo na kuongeza kuwa atashirikiana na KMPDU ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa masuala yanayoikumba sekta ya afya nchini.

KMPDU imetishia kuitisha mgomo wakati wowote ikiwa mshahara wa madaktari wanagenzi utapunguzwa hata kwa senti moja.

Haijabainika ikiwa suala hilo lilijadiliwa kwa kina wakati wa mkutano kati ya Duale na maafisa wa KMPDU.

Website |  + posts
Share This Article