Mwaura: Juhudi za kuleta amani Haiti hazitasambaratika

Tom Mathinji
2 Min Read
Isaac Mwaura - Msemaji wa serikali

Operesheni ya kuleta amani nchini Haiti, haitasambaratishwa na hatua ya Marekani ya kusitisha ufadhili. Hayo yamesemwa na msemaji wa serikali Isaac Mwaura.

Kupitia kwa taarifa leo Jumatano, Mwaura alisema operesheni hiyo inafadhiliwa na hazina iliyobuniwa chini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kufikia mwishoni mwa mwaka 2024, dola milioni 13.3 za Marekani zilikuwa zimeahidiwa katika hazina hiyo.

“Nchi za Canada, Marekani, Uturuki,Uhispani na Italia, zilikuwa zimeahidi kutoa jumla ya dola Milioni 13.3,” alisema Mwaura.

Kulingana na hatibu huyo, hazina hiyo tayari ilikuwa imepokea dola Milioni 85, huku Marekani ikitoa mchango mkubwa.

“Dola milioni 13 zilizotarajiwa kutolewa na Marekani, zinazuiliwa Kwa muda kutoka na agizo la Rais kuhusu ufadhili wa nje,” aliongeza Mwaura.

Umoja wa Mataifa ulithibitisha hatua ya Marekani kusitisha ufadhili kwa operesheni ya kuleta amani nchini Haiti, ambapo msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, alinukuliwa akisema kusitishwa kwa ufadhili huo kutaathiri msaada huo wa dola milioni 13.3

Kenya tayari imewapeleka maafisa 600 wa polisi kudumisha amani na usalama nchini Haiti, huku kikosi cha hivi punde cha maafisa 200 kikiwasili jijini Port-au-Prince Januari 19, 2025.

Nchi zingine zilizo na maafisa wa usalama nchini Haiti ni pamoja na Guatemala, Jamaica, El Salvador, Bahamas na Belize miongoni mwa zingine.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *