Afrika kuwakilishwa na timu 10 katika Kombe la Dunia

Morocco ambao watafungua mechi za kundi C dhidi ya mabingwa mara tano Brazil ndiyo timu ya Afrika iliyowahi kucheza hadi nusu fainali mwaka 2022.

Dismas Otuke
1 Min Read

Zikisalia siku saba kabla ya kuanza kwa fainali za 23 za Kombe la Dunia katika mataifa ya Mexico, Canada na Marekani, bara la Afrika litawakilishwa na timu 10.

Idadi hii ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kutokana na hatua ya kuongezwa kwa timu za Kombe la Dunia hadi 48  kutoka 32 za awali.

Wawakilishi wa Afrika ni pamoja na DR Congo inayorejea baada ya kuwa nje kwa miaka 54, Ivory Coast, Senegal, Ghana, Misri, Tunisia, Algeria, Morocco, Afrika Kusini na Cape Verde.

Morocco ambao watafungua mechi za kundi C dhidi ya mabingwa mara tano Brazil ndiyo timu ya Afrika iliyowahi kucheza hadi nusu fainali mwaka 2022.

Ghana na Senegal zina rekodi ya kucheza hadi robo fainali ya Kombe hilo, Senegal wakifikia hatua hiyo mwaka 2002 katika mataifa ya Korea Kusini na Japani,  nao Ghana wakafika nane bora mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

Je, huenda iwe mara ya kwanza kwa timu ya Afrika kufika fainali au kushinda Kombe hilo mwaka huu?

Tazama runinga ya taifa ya KBC Channel One kuanzia wiki ijayo ili kupata jawabu kamili.

Share This Article