Waziri Mbadi kuwapokea mabingwa wa Ligi Kuu Kenya,Gor Mahia

Hafla hiyo itahudhuriwa na wachezaji na maafisa wa benchi ya kifundi ya Gor Mahia.

Dismas Otuke
1 Min Read
Gor Mahia FC Crowned FKFPL Champions 2025/2026

Mabingwa wa ligi Kuu Kenya ,Gor Mahia wanatarajiwa kuwasilisha kombe walilonyakua maajuzi kwa Waziri wa Fedha, John Mbadi, mapema Alhamisi katika afisi ya Hazina kuu nchini.

Hafla hiyo itahudhuriwa na wachezaji na maafisa wa benchi ya kifundi ya Gor Mahia.

Gor walinyakua ligi kuu msimu wa mwaka 2025/2026 ikiwa taji ya 22 na kufuzu kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Mwaliko wa Gor kwa Waziri Mbadi, unafuatia mwaliko sawia na huo siku ya Jumanne ambapo walipokelewa na mlezi wao Eliud Owalo, ambaye aliituza shilingi milioni moja.

Sir’Kal, walitwaa taji ya Ligi Kuu Kenya baada ya kuzoa pointi 69,alama 5 zaidi ya Mashemeji AFC Leopards waliomaliza nafasi ya pili.

Share This Article